Mhe. Mchengerwa amwaga vifaa vya michezo shule zote wilaya ya Rufiji, aanzisha ligi ya Sensa
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji. Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za msingi na Sekondari na wanafunzi wanamichezo wote wanaoshiriki kwenye mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Mashindano ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2022 Wilaya ya Rufiji. Mhe. Mchengerwa amekabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Julai 17, 2022 kwenye shule ya Sekondari ya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji ambapo amesema ameamua kufadhili vifaa hivyo katika Wilaya ya Rufiji ili kuiendeleza michezo kwa kuwa michezo ni biashara na ajira kubwa kwa vijana. “Nimeamua kusaidia vifaa hivi kwakuwa natambua kwa sasa michezo ni miongoni mwa chanzo cha ajira na biashara kubwa duniani hivyo ni vema kufanya michezo kwa umakini mkubwa ili kujipatia ajira” amefafanua Amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu na kujituma kwa kufanya mazoezi i...