Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon na kuongoza katika mbio hizo tofauti na miaka ya nyuma ambapo mataifa mengine yamekuwa yakiongoza. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo, Februari 28, 2022 na kufafanua kuwa mwitikio huo mkubwa umetokana na kazi nzuri ambayo iliyofanywa na Rais wa Samia Suluhu Hassan toka akiwa Makamu wa Rais ambapo aliongoza kuhamasisha riadha na kuanzishwa kwa klabu za mazoezi (jogging clubs) kwenye kila mkoa hapa nchini. Aidha amesema mikakati kabambe iliyowekwa na Serikali ya sasa kwenye Sekta ya michezo inakwenda kuleta mapinduzi makubwa ikiwa ni pamoja na kutoa ajira nyingi kwa wananchi. Katika mashindano hayo mtanzania Alyce Simbu aliongoza kilomita 42 aliyetumia muda wa 02:16:30 wakati kwenye kilomita 21 nafasi ya kwanza hadi ya tatu zilichukuliwa na watanzania zikiongozwa na Emmanuel Ginniki (01:00:34), akifua...
Posts
Showing posts from February, 2022
MHE. GEKUL AELEZA MIKAKATI YA KUKUZA RIADHA KILI MARATHONI
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amewapongeza waandaji wa mbio za Kilimanjaro Marathoni huku akifafanua kwamba tukio hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Michezo nchini inayosisitiza ushiriki wa pamoja kati ya Serikali na wadau katika kuendeleza michezo mbalimbali ikiwemo riadha. Mhe. Gekul ameyasema hayo leo Februari 27, 2022 wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ili atoe hotuba yake kwenye kilele cha mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, 2022 kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi. “Sisi familia ya michezo tunajivunia uwepo wa tukio kubwa namna hii linalowaleta pamoja wanamichezo na wapenzi wa riadha kutoka katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yetu, kipekee niwapongeze Kilimanjaro Premium Lager kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza michezo hapa nchini”. Amesema Mhe. Gek...
MHE. MCHENGERWA ATEMBELEA MAONESHO YA DUBAI EXPO
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ametembelea banda la Tanzania katika Maonesho ya EXPO Dubai 2020 yanayoendelea katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu na kupongeza waoneshaji baada ya kujionea jinsi Tanzania inavyotumia maonesho hayo ya Kitamaifa kujitangaza. Mhe, Mchengerwa. jana Februari 24, 2022 amepita kukagua kwenye mabanda hayo ya maonesho na kuhimiza utoaji wa maelezo kiufasaha ili wageni wanaotembelea mabanda hayo watambue vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana nchini hatimaye wafike kutembelea Tanzania. Katika mabanda hayo, Tanzania inajitangaza kupitia fursa mbalimbali za Utalii, Madini, Nishati, Kilimo na Uwekezaji kwa wageni. Mbali na maonesho ya kuonesha fursa mbalimbali pia Tanzania kwa mara ya kwanza imeutambulisha Utamaduni wa Tanzania kupitia muziki wa singeli duniani katika maonesho haya kupitia mfalme wa singeli nchini Sholo Mwamba ambaye amewache...
MHE. MCHENGERWA ATAKA SINGELI IITEKE DUNIA DUBAI EXPO LEO
- Get link
- X
- Other Apps
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka wasanii wanaopanda leo Februari 24,2022 kuiwakilisha Tanzania kwenye Maonesho makubwa ya kimataifa ya Dubai Expo, Mfalme wa Singeli Sholo Mwamba na Mkongwe wa Muziki wa Asili wa Tanzania Mrisho Mpoto kuendelea kutoa burudani ya kukata na shoka ili kuitangaza Tanzania kimataifa. Mhe. Mchengerwa amesema haya leo Februari 24,2022 wakati ambapo Sholo Mwamba anatarajia kuendelea kuwaipagawisha dunia kwa nyimbi za singeli majira ya saa 11:00 jioni kwenye ukumbi wa *Earth Stage* baada ya kufanya vizuri kwenye onesho lake la awali Februari 22, 2022 na kuwaacha umati uiliofika kucheza naye huku wengine wakichukua picha kwa ajili ya matumizi yao. “Tunataka Singeli na muziki wa kwetu uiteke dunia ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeanza vizuri safari ya mapinduzi makubwa ya sanaa kwenye anga za kimataifa” amesisitiza Mhe. Mchenge...
Mhe. Mchengerwa awaalika wananchi Tamasha la Serengeti
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi wote kushiriki kwenye tamasha kubwa Tanzania na Afrika la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival) litakalofanyika Machi 12, 2022 jijini Dodoma ili kujionea hazina ya vipaji vya wasanii nchini. Mhe. Mchengerwa amesema haya, hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua kuwa tamasha hili ndiyo tamasha kubwa linaloratibiwa na Serikali likiwa na lengo la kuibua vipaji vya wasanii pia kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuliingizia taifa mapato kutokana na hazina ya utalii uliopo. Aidha, amesema tamasha hilo litahusisha wasanii zaidi ya hamsini wa miziki ya aina mbalimbali ambao watatumbuiza ili kuleta vionjo na radha tofauti tofauti. “Tamasha hili linaleta muunganiko wa kipekee kabisa linaloonyesha tasnia ya burudani na utalii na ndiyo maana tumetumia jina la Mbuga yetu bora Afrika na duniani ya Serengeti ili kuwavutia wageni kutoka sehemu m...
MAELEKEZO YA MHE. MCHENGERWA YAFIKIA PAZURI
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Maelekezo ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ya kutaka mchakato wa mwaka huu wa utoaji wa Tuzo za Muziki bila upendeleo yamefika mahali pazuri. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko, leo Februari 21, 2022 imeeleza kuwa jumla ya kazi 402 zimewasilishwa kuanzia Februari 9, 2022 baada ya zoezi la kuwaelimisha wadau kukamilika na kuwa BASATA limeamua kuongeza muda wa siku saba ili kutoa nafasi kwa wasanii wengi kushiriki. “Tunaongeza siku 7 kwa ajili ya wasanii kuwasilisha kazi katika vipengele vya Tuzo za Muziki Tanzania (TMA 2021)” imefafanua taarifa hiyo. Pia taarifa hiyo imefafanua kwamba mwisho wa kuwasilisha kazi hizo ni Machi mosi mwaka huu kupitia link www. tanzaniamusicawards.info Akizungumza kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Utoaji wa Tuzo za Muziki na Ugawaji wa Mirahaba kwa Wasanii Januari 28, 2022 kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Julius Nye...
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amezitaka Halmashauri zote nchini kuhamasisha programu ya kufanya mazoezi kuanzia ngazi ya mtaa ili kuimarisha afya kwa jamii na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuibua vipaji vya michezo kuanzia ngazi ya chini. Mhe. Gekul amesema hayo leo Februari 20, 2022, alipokua Mgeni Rasmi kwenye kilele cha Bonanza kubwa lililoandaliwa na Umoja wa Vilabu vya jogging klabu Mbagala, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mbio za takribani kilomita 7.5 kuanzia Mbagala hadi Mtoni Kijichi. Amezitaka Klabu za Mazoezi kote nchini kuhakikisha zinashirikisha kikamilifu makundi maalum ya jamii kwenye siku za mazoezi, huku akitoa pongeza kwa umoja wa Mbagala Jogging Klabu kwa kuandaa tamasha hilo ambalo amelielezea kuwa limekuwa la mafanikio makubwa. Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote kutenga muda kila siku kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao. “Akina mama wenzangu ujanja ...
MOROCCO YAKUBALI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KWENYE MICHEZO
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Februari 15, 2022 amekutana na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Zakaria Elgoumiri na kufanya mazungumzo ya kuendeleza sekta za michezo, utamaduni na Sanaa ambapo Balozi amesisitiza serikali yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa faida ya wananchi wa nchi hizo. Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano mzuri katika sekta hizo toka muda mrefu hali ambayo imewafanya viongozi wakuu wa nchi zote kufanya ziara na kubadilishana uzoefu wa sekta hizo. Akiwa katika kikao hicho ambacho aliambatana na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa michezo nchini Yusufu Singo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT) Neema Msitha wamekubalina na ujumbe wa Mhe. Balozi wa kuendelea kushirikiana kwenye sekta hizo. Ameyataja baadhi ya maen...
MCHENGERWA AIPONGEZA WASAFI KWA KUKUZA VIPAJI VYA WASANII
- Get link
- X
- Other Apps
John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza Kampuni ya Wasafi kwa kukuza sanaa ya muziki na kuzalisha ajira kwa vijana wengi hapa nchini. Akizungumza kwenye hafla ya Usiku wa Mahaba Ndi Ndi Ndi siku ya wapendanao Februari 14, 2022 jijini Dar es Salaam amesema Wasafi ina mchango mkubwa katika kuibua na kukuza vipaji vya wanamuziki. " Naomba nikuhakikishie Serikali ipo pamoja na nyie katika kukuza sanaa " amesema Mhe.Mchengerwa Aidha, amesema Serikali inakwenda kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wasafi mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji hadi mkoa kwa mkoa kutafuta vipaji vya wasanii lengo ni kuwashindanisha na kuwaendeleza. Ameongeza kuwa, wizara inakwenda kuendeleza mapinduzi ya ukuzaji wa Sanaa ili kutoa ajira zaidi kwa vijana katika ngazi ya kitaifa na kimataifa. Amefafanua kwamba kufanya hivyo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kutaka kuboresha sekta hiyo ili wasanii nchini waweze kunufaika na kazi zao. Kwa upande...
Mhe. Mchengerwa apongeza ubunifu wa wadau wa tamasha la Sauti za Busara
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewapongeza wadau mbalimbali wa Sanaa walioshiriki kwenye tamasha la Sauti za Busara Zanzibar kwa ubunifu wao na kuwataka waendelee kutumia matamasha hayo kutangaza bidhaa na huduma wanazozitoa. Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo alipotembelea mabanda yaliyokuwa yakionesha bidhaa na huduma zao kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Februari 13, 2022. Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Mhe. Simai Mohamed Said ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kutembelea wadau wa tamasha hilo huku akisisitiza kuwa kitendo hicho kimeonesha anathamini mchango wa wadau hao. Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, Sinai Mohamed Said akimtambulisha Mhe. Mchengerwa kwa mmoja wa wadau kwenye banda la Benki ya CRDB Mhe. Mchengerwa akiwa na kikosi cha mfalme wa Singeli nchini Sholo Mwamba kabla ya kikosi kupan...
Mhe. Mchengerwa aikaribisha dunia Tamasha la Serengeti kupitia Sauti za Busara
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha kubwa la kimataifa la Sauti za Busara kutoka sehemu mbalimbali duniani kushiriki kwenye tamasha la kihistoria la muziki la Serengeti litakali fikia kilele chake Machi 12, mwaka huu jijini Dodoma. Akizungumza kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara usiku wa kuamkia leo Februari 14, 2022 huko zanzibar amesema Serikali inakwenda kuandaa matamasha makubwa ya kihistoria ambayo yataonesha utamaduni wa kitanzania, hivyo dunia inakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria na kimataifa. "Naomba kutumia nafasi hii kuwakaribisha kwenye Tamasha la Serengeti na Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo ambayo yanakwenda kuionyesha dunia utajiri wa utamaduni na vivutio vya utalii duniani". Ameongeza Mhe....
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Februari 13, 2022 anatarajia kushiriki kwenye kilele cha Tamasha la kimataifa la Sauti za Busara la mwaka huu jijini Zanzibar. Tamasha la Sauti za Busara ni miongoni mwa matamasha makubwa nchini ambayo yamefanikiwa kuonesha utamaduni wa nchi Tanzania duniani kupitia Sanaa za muziki. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi ambaye anashiriki amesema tamasha la mwaka huu limeboreshwa zaidi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Aidha, amesema kutokana na tamasha hili amejifunza mengi ambayo yanaweza kusaidia kuboresha matamasha yanayokwenda kuandaliwa hivi karibuni. “Tumejifunza mengi katika tamasha hili, tutatumia, kazi iliyombele yetu ni kubeba mambo mazuri ya tamasha hili kuboresha matamasha yanakuja mbele yetu yawe kwenye hadhi ya kimataifa ili kuitangaza Tanzania na kuuza utamaduni wetu duniani kama tulivyo elekezwa na Rais wetu kipenzi, Mhe. Samia Suluhu Hassan”. Ameo...
MHE. MCHENGERWA AMTEMBELEA PROF JAY MUHIMBILI
- Get link
- X
- Other Apps
Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa amemtembelea aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule (Prof. Jay) anayetibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mhe. Mchengerwa amefika leo Februari 12, 2022 kumjulia hali msanii huyo na kuwasilisha salamu za Serikali kama msimamizi Mkuu wa Sekta ya Sanaa hapa nchini. “Nimefika kumjulia hali mmoja wa wadau na miongoni mwa wasani ambao tunatambua na kuthamini mchango wa kazi zake za sanaa ambazo zimehamasisha vijana wengi kujiajiri kupitia Sanaa ya muziki hapa nchini". Ameeleza Mhe. Mchengerwa Tayari Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema itagharamia matibabu yake hadi hapo ataporuhusiwa kutoka hospitalini hapo. Kwa upande wake mke wa Prof. Jay, Bi. Grace Mgonjo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa upendo wa kuja kumwona msanii huyo . Pia ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwapokea na kuwahudumia...